11 Agosti 2024 - 14:26
Ansarullah: "Inaonekana kwamba Serikali za Kiarabu hazioni wala hazisikii"

Ofisi ya Kisiasa Kisiasa ya Ansarullah imezituhumu Serikali za Kiarabu na Kiislamu kwa kukaa kimya na kujifanya hazina uwezo wa kufanya lolote kuhusiana na jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni, na ikatangaza ikisema: "Ni kama kwamba nchi hizi hazioni wala hazisikii."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ilitoa taarifa yake ikitangaza kuwa: "Tunalaani vikali hatua mpya ya kikatili ya utawala ghasibu wa Israel katika kuwashambulia Waumini wa Kipalestina katika Shule ya al-Tabeen huko al-Darj, ndani ya eneo la Ukanda wa Gaza, ambapo shambulizi hilo lilisababisha kuuawa kwa zaidi ya raia 100 wa Palestina.

"Utawala wa Kizayuni unaendelea kufanya mauaji ya umwagaji damu na ambao ni umwaga damu usio kuwa na kifani kwa raia wasiokuwa na silaha wa Palestina.

Ofisi hii imeongeza kuwa: Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah ilizituhumu zaidi Serikali za Kiarabu na Kiislamu kuwa zimenyamaza kimya na kujifanya ni hazina uwezo wa kufanya lolote kuhusiana na kukomesha jinai zinazoendelea za utawala huo ghasibu wa Kizayuni, na ikabainisha na kutangaza bayana kuwa: "Nchi hizo sambamba na jinai za utawala huo ghasibu wa Kizayuni, ni kama hazioni, wala kusikia! Na wala hawasemi chochote!